GET /api/v0.1/hansard/entries/1216313/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1216313,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1216313/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Ni ukweli kuwa wanyama wamekuwa wanasumbua watu huko Laikipia. Tumeandika taarifa tukiuliza hayo maswali. Ukitembelea sehemu za Sironi unapata watu wameshambuliwa na ndovu na kuuawa. Mimea yetu yote imeharibiwa na ndovu. Katika sehemu ya Manguo viboko wanashambulia watu. Mwenyekiti ambaye ni Seneta kutoka Kaunti ya Nyandarua, Sen. Methu, nimemskiza katika mikutano mingi akisema kuwa yeye ni kiongozi wa wanyama. Lakini inaonekana hawa wanyama wamemlemea. Sen. Methu anafaa kutumia lugha anayoelewa vizuri kwa sababu amekuwa akituambia katika kila mkutano kwamba yeye ni mwenyekiti wa mazingira na wanyama wako chini yake. Sijui sasa kama wanyama wamekaa juu yake kwa sababu sasa amenyamaza kimya. Leo tunamuomba Sen. Methu aongee kuhusu viboko na wanyama hawa ili atueleze kiasi ya kazi ambayo amefanya kwa sababu wanyama wale wanatusumbua sana. Katika Kaunti ya Laikipia, kama si kiangazi ni wanyama wanatusumbua na kama sio wanyama ni majangili wanaotuibia. Tunamgojea Sen. Methu kwa hamu na ghamu atujibu ili tutosheke. Asante, Bw. Spika."
}