GET /api/v0.1/hansard/entries/1216329/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1216329,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1216329/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, jana uliongea na ukasema ya kwamba mavazi ambayo hasa ni ya Kiafrika tunapaswa tuyatilie mkazo. Hii ni kwa sababu utamaduni wetu unafaa zaidi na tuweze kuutukuza. Ni kama vile ninavyoongea Kiswahili. Wengine wanasema ya kwamba sipaswi kuongea Kiswahili kwa sababu mtu anayeongea Kiswahili ni kama hajaelemika vilivyo. Anapaswa aongee lugha ya nyani ambayo ni Kiingereza. Sen. Chimera, ako sawasawa. Ijapokuwa sitaki kukwambia uamuzi utakaotoa, lakini, kwangu mimi na wengi walioko hapa, hata mwenzake wakili wa kutoka Kaunti ya Makueni anakubaliana na mimi kwa sababu anaona vizuri."
}