GET /api/v0.1/hansard/entries/1216635/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1216635,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1216635/?format=api",
    "text_counter": 392,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kila nchi iko na vyama lakini katika Ufalme wa Mbinguni, vyama ni viwili; cha Yesu Kristo na cha shetani. Kutoka nyakati za mababu zetu, watu wengi walikuwa wanahubiri mambo ya Mt. Kenya. Tulipozaliwa na kuwa wakubwa, hatukusikia wakiongea mambo ya mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke. Mambo ya Yesu Kristo yakaja. Tukahubiriwa na ikawa sasa ni Ufalme wa Mbinguni na shetani. Ufalme wa Mbingu ni Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu. Wale majaji ambao walifunzwa na wazazi wao, hawakufunzwa mambo ya giza. Sasa hivi, wanataka kufunza watoto wetu mambo ya mwanaume kwa mwanaume. Hili jambo linaibuka wakati ambapo kazi zimekosekana, madawa ya kulevya na usherati umekithiri na dunia imeharibika. Wanatuletea mambo mengine ambayo in ya giza, ilhali vijana hawana kazi. Wanataka kutufundisha kwamba hivi karibuni, tutasomesha watoto wetu hadi kiwango cha shahada, halafu wakose kazi na waanze mambo ambayo hayafai. Kazi yao itakuwa kukatana panga na vita vya usiku na mchana. Kama Seneta wa Kenya kutoka Kaunti ya Embu, ninaunga mkono kwamba hawa majaji wachunguzwe vizuri. Walikuwa na fikira zipi? Je, nia yao ni kutaka kuharibu Kenya? Hakuna mtu hata mmoja nchini Kenya anayejua mambo ya Yesu Kristo, ambaye anaweza kuunga mkono hayo maneno."
}