GET /api/v0.1/hansard/entries/1217773/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1217773,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1217773/?format=api",
    "text_counter": 313,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa hakika sisi tunaheshimu mahakama lakini hatuwezi kubali hukumu ambazo zimetolewa zitakazo athiri jamii zetu. Tunajua hivi sasa kabla ya hawa wanaojiita LGBTQIA+ kupata vibali vya kutengeza makundi yao na kutambulika katika taifa letu, kumekuwa na tetesi na hatari nyingi sana za mambo haya yaliyo kinyume na dini na tamaduni zetu. Kwa wakristo katika Bibilia tunajua habari za Sodom na Gomorrah. Katika Kiislamu ni vile vile. Je, leo watu hawa tukiwapa kipaumbele ama jukwaa ambalo watatumia kuendeleza mambo yao maovu, na machafu ambayo ni dhambi, taifa hili la Kenya tutakuwa tunasonga wapi? Lazima tuangalie takrimu za idadi ya Wakenya inavyoendelea kwa sababu pia tumekumbwa na majanga mengi na maradhi kama vile COVID-19, saratani nakadhalika. Hivyo basi, lazima tuangalie takwimu kuhusu idadi ya Wakenya na jinsi tunavyoweza kuongeza idadi hiyo. Leo hii tunaambiwa kwamba hawa watu watakuwa na uwezo wa kuunda kundi lao waweze kuendeleza hoja zao. Pengine swali tutauliza ni hili: wakiwa na makundi kama hayo, hoja zao zitakuwa ni zipi? Bila shaka hoja zao ni kwamba, “Oh sisi tumetengwa”. Mmetengwa vipi? Wewe ukiwa Mkenya, mume ama mke haki zako zote za kimsingi ziko katika Katiba na zimeangaliwa. Iwapo watasema wanataka makundi yatetee haki zao, tunajiuliza hizo ni haki gani? Kwangu mimi hizo sio haki bali ni upotevu na ni dhambi kubwa ambazo tunataka kuidhinisha katika nchi hii. Tunajua makundi haya yamekuwa yakifanya kazi kisiri. Yamekuwa yakifanya kile tunasema kwa Kingereza awareness na recruitment . Yamekuwa yakisajili watu katika makundi yao ili kuwaingiza katika tabia potovu kama hizi. Leo tukiwapatia ruhusa mwafaka ya kisheria kwamba wanayo nafasi ya kuunda makundi haya ama majukwaa haya na waweze kuzungumza mambo yao ambayo wanayahitaji, je, taifa hili la Kenya tutakua katika hali gani? Nataka kumwona kiongozi wa taifa hili akizungumzia suala hili na kulikemea. Kama anavyosema yeye ni mkristo ambaye ameshika dini sana na iwapo ni mkristo kweli ameshika dini sana, tunataka kusikia sauti yake na tunataka kusikia sauti ya taifa zima la Kenya likikemea jambo hili. Tunajua ya kwamba ulimwengu umebadilika na kwamba kuna mambo mengi ambayo lazima yawe yamebadilika. Ingawa hivyo, hatutakubali kubadilika kiwango cha kwamba tutakwenda kinyume na dini zetu na maadili yetu kama taifa. Ukiangalia Katiba yetu kuna sura ambayo imezungumzia maadili ya kitaifa. Je, katika maadili ya kitaifa, mmeona mambo ya wasagaji na mambo ya mashoga? Pole kwa sababu lugha hii pengine itakua ni lugha potovu lakini ndivyo inavyoitwa katika Kiswahili. Mwanaume kwa mwanaume itakuwa ni mashoga, Mwanamke kwa mwanamke itakuwa ni masago. Tunajua kuwa watu hawa na haya mambo wanayoyafanya ni mambo mabaya ambayo yanatuletea maradhi, haswa wasagaji. Vifaa wanavyotumia vinaleta saratani za kizazi katika kina mama. Jambo hili hatutalikubali. Iwapo watu wetu wataiga tabia hizi na ziwaingie katika nafsi zao, basi itakuwa mtoto wa kike hatapata mume wa kumuoa na mtoto wa kiume pia hatapata mke wa kuoa. Kwa sababu athari huanza pole pole. Unapoona moshi ujue moto upo njiani waja na wakati. Je, tutaweza kuzima moto wa dhambi hizo? Watoto wa kiume tunawaenzi, vile vile wa kike ndiposa Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam, alimtoa Hawa kutoka kwa Adam ili tuweze kuzaa na kuweka ulimwengu wetu katika hali ya usawa. Jamani tunataka kusikia sauti ya Rais ikikemea jambo hili. Tunataka kusikia sauti za Mawaziri na vitengo vyote vya Serikali. Wabunge wenzangu tukemee jambo hili. Jambo hili likikubaliwa basi sisi tumeangamia na umma pia umeangamia. Hatutaweza kuwa na watoto wa kike wala wa kiume. Maanake kama mtoto wa kiume atavaa kama mtoto wa kike, na atake kuziiga mpaka tabia za kike, je, sisi tutakuwa na watoto wa kike tofauti na wa kiume kweli? Hilo ni suala nyeti kwa hivyo tutafakari ya babu. Tujiangalie, tujinasue, na tujiulize kama taifa hata kama tunataka kusaidika…."
}