GET /api/v0.1/hansard/entries/1217877/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1217877,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1217877/?format=api",
    "text_counter": 417,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda, kwa kuniruhusu niweze kupenyeza sauti yangu kwa suala hili. Nitafanya haraka kwa sababu ya muda ili wengine wapate nafasi ya kuchangia. Kwa kweli, inasikitisha sana Mahakama Kuu kuidhinisha kusajiliwa kwa vyama hivi vya usagaji na ushoga ama uhanithi. Mimi nitawasihi majaji hao wamche Mwenyezi Mungu. Hapa duniani tumekuja kulima shamba ambalo matunda yake tutayapata mbeleni. Kwa hivyo, lolote wanalolifanya na maamuzi yote wanayoyatoa hivi sasa watakutana nayo mbele akhera, ambapo wote wataondoka katika ulimwengu huu. Hakuna mtu atabaki. Pia wajue kwamba wataweka kumbukumbu za vizazi vilivyoko na vitakavyokuja kulingana na maamuzi ambayo wanayafanya sasa. Nchi hii ni nchi ya watu wanomwabudu Mungu. Leo hii tunalazimishwa kumuabudu shetani. Ikiwa sasa hivi tunaabudu Mungu na ukame ndio huu, je huku tunakoelekea si kutatokea maafa ambayo hatutayaweza sisi? Mila na maadili yetu ya Kiafrika haituruhusu kushangilia utovu huu wa nidhamu. Ushoga haukubaliki Afrika na pia haukubaliki na dini zote. Kwa kweli, nchi za Magharibi zinatumia umaskini wetu kutulazimishia mambo wanayoyataka. Tusiwakubalie. Tuje pamoja kama Taifa tukemee haya. Dini zote zisimame kuelimisha waumini wao kuwa njia hii ni ya shetani. Tusikubali kuelekea waliko wao. Wametufundisha kutemebea uchi, wengine wakaiga na sasa wanataka kutuingiza kwa shimo kwa kuleta ushoga. Mwisho, Jumba hili la kutunga sheria, ikiwa mtakubali, kutakuwa na Spika moja shoga akae pale na kujipaka rangi mdomoni Hapo tutakuwa tumelimaliza kabisa Taifa nzima. Tusimame imara tupinge hili jambo. Ahsante Mhe. Spika wa Muda."
}