GET /api/v0.1/hansard/entries/1217889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1217889,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1217889/?format=api",
"text_counter": 429,
"type": "speech",
"speaker_name": "Molo, UDA",
"speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
"speaker": null,
"content": " Nashukuru sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa muda huu kuongeza mawazo yangu katika mjadala huu. Kwa sababu ya huu uamuzi wa Mahakama ya Upeo, nilijiuliza: “Kwa nini wale ambao waliandika Katiba yetu walitupa mikono mitatu ya Serikali; ile tunaita Executive, Bunge na Mahakama?” Baada ya Bunge kupitisha Mswada, lazima uende kwa Mheshiwima Rais kutia sahihi ndio uwe sheria. Kama Mheshimiwa Rais anadhani, kwa vyovyote vile, kwamba huo Mswada haufai, anaweza kuurudisha kwa Bunge ili Bunge lifikirie tena hilo suala. Hata baada ya Mheshimiwa Rais kusema kwamba huo Mswada ni sawa na atie sahihi kuwa sheria, Mkenya yeyote anaweza kwenda kortini ili hiyo sheria iwekwe kando. Tukiangalia vile Executive inafanya kazi yake, lazima ikuje hapa Bunge kuomba Bajeti. Hata wakitumia pesa vile Kipengele cha 223 ya Katiba kinavyoruhusu, sisi tuko na uhuru wa kukataa yale ambayo yamefanywa. Wakati jambo limepita katika ile Mahakama ya Sheria, ikaenda High Court na baadae Supreme Court ikatoa uamuzi kama huu ambao hauendanishani na maadili ya kijamii, tunafaa kufanya nini kama wakenya? Ni jambo ambalo hili Bunge linafaa kujadili. Mhe. Lilian Kogo aliongea kuhusu sheria ambayo walipitisha mambo ya ugawaji wa mali katika ndoa. Kama imefanywa na Supreme Court na mtu akadhania haijamfurahisha kulingana na Katiba yetu, anafaa kutatufa suluhu wapi?"
}