GET /api/v0.1/hansard/entries/1217893/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1217893,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1217893/?format=api",
"text_counter": 433,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, PAA",
"speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": " Mhe. Spika wa Muda, nakushukuru kwa sababu ya kunipa nafasi hii. Kwa haraka, ningetaka kulaani vilivyo uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu kwa sababu ni chanzo cha upotuvu wa jamii. Mwanadamu alipokuja katika ulimwengu huu, alipewa vitabu viwili: Bibilia na Quran. Naye akajiongezea Katiba. Kile kilichotengenezwa na mwanadamu sasa kimekosa kuheshimiwa mpaka imefika mahali tunapelekwa ambako siko. Mhe. Spika wa Muda, hebu fikiria kidogo utoke hapo uliko na utakapofika nyumbani, mtoto wako anakuletea mwaliko unaosema kuwa Jumamosi ataolewa na mwanaume mwenzake. Utawaambia nini Wajumbe wenzako ukifika hapa? Ni jambo la aibu sana. Kwa hivyo, tunalilaani vilivyo. Nimemuuliza Mhe. Bedzimba kuwa Ijumaa ni siku ya maombi. Tunafaa kufanya kunuti kwenye Misikiti na Makanisa juu ya hao majaji. Mungu atuwezeshe tupate majibu kwa sababu maamuzi kama haya ni ya kutumaliza kwa njia nyingine ya mlango wa nyuma."
}