GET /api/v0.1/hansard/entries/1218008/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218008,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218008/?format=api",
    "text_counter": 95,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, UDA",
    "speaker_title": "Hon. (Dr) Robert Pukose",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuchangia Hoja ambayo imeletwa na Mhe. Thuddeus Nzambia, Mjumbe wa Mwingi Kaskazini. Pole, naomba msamaha, Mjumbe wa Kilome. Nataka kumshukuru kwa kuleta Hoja hii ambayo inazungumzia malipo ya uzeeni. Mara ya mwisho wazee walisajiliwa ilikuwa 2016. Wajumbe wengi wanapoenda nyumbani wanaulizwa na wazee kuhusu pesa za wazee. Hali ni kwamba wazee wengi ambao wametimu umri wa miaka sitini na tano kuendelea hawajasajiliwa. Huo ndio mjadala mkubwa kule mashinani. Ninafikiri hili Bunge litaunga mkono hii Hoja inayosema kwamba kusajiliwa kwa wazee kufanyike kila wakati. Kila mtu anazaliwa wakati tofauti, kwa hivyo wanafika umri wa miaka sitini na tano wakati tofauti. Mambo ya kusajili inafaa kufanyika kila wakati. Ofisi ya huduma za jamii, kwa mfano, katika Eneo Bunge langu la Endebess, pale karibu na ofisi ya Mkuu wa Wilaya, pawe pakifanyika usajili kila siku. Wale wafanyikazi wa serikali wanapoandikwa, wanapokea mshahara lakini hawatimizi jukumu lao la usajili. Mzee mmoja anaposajiliwa na mwingine akose, inachangia katika ufisadi kwa sababu wengine wanasajiliwa na wengine kuachwa. Kwa mfano, usajili ulifanywa 2016, sasa ni 2023, takriban miaka saba iliyopita. Mambo haya yanachangia katika ufisadi. Ndio maana unapoenda mashinani, kuna wale wazee wanaopokea marupurupu na kuna wale ambao hawapati na wanaumia. Malipo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}