GET /api/v0.1/hansard/entries/1218009/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218009,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218009/?format=api",
    "text_counter": 96,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, UDA",
    "speaker_title": "Hon. (Dr) Robert Pukose",
    "speaker": null,
    "content": "haya yanafaa kulipwa kwa wakati ufaao na kwa njia inayofaa. Wakati mwingine wazee wanapoenda kwenye foleni ya kupokea marupurupu, huwa ndefu. Wao hulazimika kwenda kupiga foleni mapema na mwishowe kuhisi njaa wakingojea. Ni shida kubwa. Wazee wanangoja kupata marupurupu ambayo huja baada ya miezi sita. Kufikia wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, marupurupu haya hayakuwa yanalipwa. Serikali ya Rais William Ruto ndiyo imeanza kuwalipa. Wakati huo kila ulipoenda mashinani, ungewapata wazee wengi wakilia njaa na shida nyingi. Ninafikiri hili jambo ambalo limeletwa na Mhe. Nzambia ni nzuri. Tunataka Bunge liamue na pesa iwekwe na Kamati ya Bajeti kwa wakati mzuri. Serikali pia izingatie suala hili kwa njia nzuri ili wale wazee wote ambao wanahusika waweze kuwekwa kwa orodha na waanze kupata marupurupu mara moja. Ninashukuru kwa nafasi ya kuchangia Hoja hii. Ninaunga mkono Hoja hii na ninataka Bunge hili liipitishe haraka ndiposa Serikali itenge pesa na wazee walipwe."
}