GET /api/v0.1/hansard/entries/1218011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218011,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218011/?format=api",
    "text_counter": 98,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Keiyo Kusini, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Adams Korir",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Sana, Mhe. Spika wa Muda. Vile vile ningependa kuchukua nafasi hii kuchangia Hoja hii ya uandikishaji wa pesa za wazee katika jamii. Ningependa kumshukuru sana Mhe. Nzambia kwa kuleta Hoja hii. Kama tunavyojua sote, uchumi wa taifa letu uko katika hali ngumu. Kwa kweli, wazee wetu ambao walifanya kazi nyingi ya kujenga taifa wanapitia mazito. Pesa hizi zitawasaidia ili kuhakikisha wanajikimu maslahi yao kama vile vyakula, dawa, kusaidia jamii yao na matumizi mengine mengi. Wakongwe katika jamii yetu hawapewi kipaumbele na baadhi ya jamaa zao. Kwa hivyo, pesa hizi zitawasaidia sana kukimu maisha yao. Kule mashinani baadhi ya maswali ni haya: Ni lini tutapewa pesa hizi ili tuweze kujisaidia? Kwa mfano, katika Eneo Bunge langu la Keiyo Kaskazini, wazee wengi wanauliza ni mtindo upi unaotumiwa kubagua yule anayehitimu na asiyehitimu? Tunafaa kuangalia suala hili ili tuweze kuwanufaisha wote ambao wamefika miaka sitini na tano na zaidi. Ningependa pia kuunga mkono mchango ambao ulitolewa na Mheshimiwa mmoja, kwamba iwapo tunataka kuwasajili wazee na kuhakikisha kuwa wanapata pesa hizi sharti tujiulize: Ni mpango upi utawekwa ili kuhakikisha wale wanaostahili kupata hela wasivamiwe? Pendekezo nzuri ni kwamba ni vizuri kuhusisha watawala kama machifu, na wazee wa mtaa kuwalinda. Ningependa kuunga mkono Hoja hii kwa sababu hizi pesa zitawezesha familia za wazee kuwatunza kwa heshima na hadhi wanayostahili. Tuko katika jamii ambayo bila pesa ya kujilinda, maisha ni magumu. Kwa hayo na mengine mengi, ninaunga mkono Hoja hii."
}