GET /api/v0.1/hansard/entries/1218029/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218029,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218029/?format=api",
    "text_counter": 116,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kitui South, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr) Rachael Nyamai",
    "speaker": {
        "id": 13374,
        "legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
        "slug": "richard-ken-chonga-kiti"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Thuddeus Nzambia, Mbunge wa Kilome. Nataka kumshukuru sana kwa sababu amekuwa akileta mijadala ambayo inasaidia wananchi. Pia amekuwa akifanyia watu wa Kilome kazi nzuri sana. Mimi kama Mbunge wa Kitui Kusini, jambo hili la kuendelea kuandikisha watu ambao wamefikisha miaka 70 ni jambo muhimu sana kwa wananchi wa kwangu wa kaunti ndogo za Ikutha na Mutomo. Mara ya mwisho watu walisajiliwa ilikuwa ni mwaka wa 2016 wakati tulikuwa tunakaribia uchaguzi. Wale ambao walikuwa miaka 69 wakati huo, saa hii wamepitisha miaka 77. Ninaunga mkono kwamba hawa watu wanafaa kusajiliwa mara moja kupitia kwa maeneo Bunge sana sana yale yako na zaidi ya kaunti ndogo mbili kama vile eneo Bunge langu. Utapata kwamba katika eneo Bunge langu la Kitui Kusini wazee hawasajiliwi katika kaunti ndogo ya Ikutha ama ya Mutomo. Miongoni mwa hawa watu, wengine wamezeeka hata hawaskii na wengine hawaoni. Kwa hivyo, hii inafaa ipelekwe katika kaunti ndogo, kata, kata ndogo hadi chini kwa wazee wa mtaa. Kama hawajajua, wafikishiwe habari hiyo. Jambo lingine muhimu sana ni kuweka pesa ya kutosha. Machifu na manaibu wao wasibague wazee ambao wanapaswa kufaidika kutokana na huu mpango. Tusipozingatia hilo, inamaanisha kwamba wazee wanaweza kutengwa kama hawana watu wa kuwatetea. Jambo lingine ni kuhakikisha kwamba wazee wote wale wako katika mradi huu wameingizwa katika NHIF. Nataka kushukuru sana NHIF kwa sababu wanatibu magonjwa kama vile saratani, na wanafanya upasuaji spesheli yaani specialised surgery . Hii ni kwa sababu hawa wazee ndio wako na hizo shida ambazo zinahitaji upasuaji. Aidha wanahitaji madawa ya magonjwa yanayowapata. Tunapoweka pesa katika mradi huu tukumbuke kwamba Ksh2,100 hazitoshi. Mbunge wa Kipkelion West na Mhe. Thuddeus Nzambia wamesema kwamba hizi pesa hazitoshi na ni vizuri ziongezwe kupita Ksh3,000. Hivyo, nia iliyowekwa na waanzilishi wa mradi huu itakamilika. Na sasa kwa sababu tunampatia Mheshimiwa Rais kipaumbele katika kufanya kazi yake, ninataka kama Mbunge wa Kitui Kusini kumwambia aangalie sana mambo ya wazee kwa sababu wanahitaji mpango huu wa uzeeni. Huu mpango unawawezesha kupata mahitaji yao ya kila siku hasa dawa. Pia wanawezeshwa kuzuru sehemu mbali mbali jambo ambalo linawapa maisha marefu. Mhe. Spika wa Muda, utakumbuka kwamba mtu ambaye anangojea kitu anaweza kuishi muda mrefu. Unapongojea mwisho wa mwezi ufike ili upate Ksh2,000 hiyo inaweza The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}