GET /api/v0.1/hansard/entries/1218130/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218130,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218130/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Ninaunga mkono Hoja hii iliyoletwa na Mbunge wa Kilome, Mhe. Nzambia. Ni muhimu uendelezi wa kusajilisha wazee ufanyike. Pia, Mhe. Nzambia ameleta Hoja hii kwa wakati mufti. Kuanzia mwaka wa 2007 hadi 2016, wazee wengi waweza kuwa walifariki na ni lazima usajilishaji endelevu uweze kuanza tena ili kusafisha orodha ile ya wazee. Wazee hawa ni kina baba, mama na ndugu zetu wakubwa ambao wamehitimu miaka 65. Maisha yamekuwa magumu. Ningependelea umri huu ushukishwe hadi miaka 60. Kufika miaka 70 hapa Kenya imekuwa changamoto sana. Wazee wanakufa njaa. Hakuna maji na mifugo inakufa. Ni maisha mengi sana ambayo yanaishia miaka 50 au 55. Ibara ya 57 ya Katiba yetu imeeleza wazi jinsi ya kuaangazia changamoto ambazo zinawakumba wazee wetu katika maisha yao ya uzeeni. Ni haki yao ya kikatiba wazee hawa waweze kuangaziwa haswa kwa chakula, fedha na hata makao. Wazee wengi wanaishi maisha ya uchochole, hawana nyumba na wanaishi tu vibandani. Ni wakati mzuri katika uangalizi wa wazee wetu na katika Bunge hili iwezekane kuwa wanapata makao bora. Serikali ilikuwa imetenga Ksh2,000 kila mwezi lakini wakati huu haitoshi kununua hata bandari ya unga. Na kama hainunui bandari ya unga, basi hamna pesa za mboga. Kwa hivyo, mwaka wa 2007 in kitambo sana tangu pesa hizi ziamuliwe. Ni vyema zifikishwe hata Ksh5,000 ili waweze kununua bandari ya unga, mboga kama maharagwe, pojo au omena . Pia, ni wajibu wetu kuangazia afya ya wazee hawa. Vyakula wanavyokula si sawa na vile tunavvyokula. Kwa hivyo, hali ya afya yao na vyakula vyao viweze kuangaziwa vizuri. Katika Kaunti yangu ya Kilifi, Ganze, Magarini na Kaloleni wako mbali sana na maafisa wanaotumika katika uhamishaji wa fedha kidijitali yaani cash transfer. Nilipokuwa Mwakilishaji wa Wodi pale Kibarani kule Kilifi mwaka wa 2013, nilikuwa naona wardadministrators wakihusishwa sana kuona wazee wamelipwa pesa hizi hadi kule vijijini. Tumesikia hapa kuwa mzee wa miaka 80 au 90 hawezi kutembea kuenda benki ambapo malipo haya hufanyika. Kaunti ya Kilifi, benki nyingi ziko Kilifi Mjini, Malindi, Mariakani, Kaloleni na Mtwapa ambapo ni Kilifi Kusini. Kwingine, benki ziko mbali. Tunapaswa kuona ni mikakati ipi itawekwa ili pesa hizi zifikie wale wazee binafsi maanake hata next of kin wanaotumwa kuwachukuliwa pesa hizi hawazifikishi. Pesa nyingi huishia mikononi mwa wale waliopendekezwa kuchukulia wazee pesa hizi. Mhe. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii ili tuone ni vipi Kamati husika itaweza kuhakikisha kuwa pesa hizi zinafikishwa na wahusika kwa wazee waliolengwa ili waweze kusaidika. Ahsante Mhe. Spika wa Muda."
}