GET /api/v0.1/hansard/entries/1218132/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218132,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218132/?format=api",
    "text_counter": 219,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Igembe South, UDA",
    "speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante Mhe. Spika wa Muda. Nami ningependa kuchangia Hoja hii. Ninampa hongera sana Mhe, Nzambia kwa kuileta Bungeni. Wazee ndio wametulea hadi mahali tumefika leo. Ni muhimu sana sisi kama Wabunge kuangalia na kutilia uzito jambo hili la malipo ya wazee. Usajili wa wazee ulifanyika mwaka wa 2016 na kufikia sasa, haujafanyika tena. Ndio maana namshukuru sana Mhe. Nzambia kwa kuleta Hoja hii ili iweze kujadiliwa katika Bunge hili na ili pia sauti zetu ziweze kusikika Serikalini na kuhakisha kwamba wazee wanasajiliwa na pia wanapata hela kila mwezi. Kulingana na mambo yalivyo sasa, hizi hela za wazee hukaa zaidi ya miezi miwili au mitatu kabla ya hawa wazee kuzipokea. Ikumbukwe kwamba wengi wao hawana makao na wengine ni wajane. Kwa hivyo, hawana watu wa kuwashughulikia. Ni vyema sana wazee hao wapokee malipo yao baada ya mwezi mmoja. Vilevile na kulingana na hali ya maisha yalivyo wakati huu, ni vyema hizi hela ziongezwe ili hao wazee waweze kujikimu kimaisha. Mambo mengine yanahitaji hela nyingi ili mtu aweze kuishi vizuri. Ni vyema kuangazia nyongeza ya hizi hela."
}