GET /api/v0.1/hansard/entries/1218133/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218133,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218133/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, UDA",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": null,
"content": "Katika msururu wa usajili, kunakuwa na mambo mengi. Wazee hawa wa miaka mingi hupitia mambo mengi ili wasajiliwe. Wengine wanaosajiliwa ni marafiki wa wale machifu ambao wanafanya usajili. Ni vyema kila mtu ama kila mzee ambaye anasajiliwa, asajiliwe bila ubaguzi wakati wa usajili. Wakati mwingine, wazee wanaofaa kunufaika na hela hizi wanaachwa nje sababu sio marafiki wa wale wanafanya usajili. Wakati mwingine wanaonekana kama wametoka familia duni sana ambazo hazifai kuangaliwa. Familia hizi ndizo tunataka ziangaziwe sana. Kwa hivyo, ni lazima kuweka mikakati inayofaa kuhakikisha wanaofaa kunufaika wamesajiliwa."
}