GET /api/v0.1/hansard/entries/1218134/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218134,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218134/?format=api",
"text_counter": 221,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, UDA",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": null,
"content": "Wale ambao wanatumika kuchukulia hela wazee wasiojiweza kufika katika benki zetu huwa wanapotea na pesa zile, ama wanawaibia. Ni vizuri kuwe na mikakati ambayo itatumika kuwachukulia hatua kali wanaohusika kuwaibia hao wazee. Hela tunazozungumzia ni za kusaidia hao wazee ili waweze kuendelea vyema kimaisha. Mambo haya yameangaziwa katika Katiba. Ni jukumu letu kuhakikisha hao wazee wamehudumiwa vyema na wamepata hela hizi ili maisha yao yaendelee vyema."
}