GET /api/v0.1/hansard/entries/1218135/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218135,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218135/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, UDA",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": null,
"content": "Jambo lililonisukuma sana kuzungumzia mambo haya ni kwamba, mara kwa mara ninapozunguka katika Eneo Bunge langu la Igembe Kusini, wazee huniuliza mbona usajili hauendelei hadi sasa. Ndio maana nahimiza Serikali kwamba kuwe na usajili wa hawa wazee mwaka baada ya mwaka kwa sababu wanaendelea kuzeeka miaka isongapo."
}