GET /api/v0.1/hansard/entries/1218148/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218148,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218148/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii adimu niweze kuongea na kusikika katika kumbukumbu za Bunge hili la 13 nikitetea haki za wale wazee wanyonge walio kule nyanjani. Ni juzi tu tulikuwa tukitembea katika safari ya kisiasa ya kutuwezesha kufika katika Bunge hili la kitaifa. Wazee walikuwa wakinililia na kuniambia, “Mhe. tutakupeleka Bungeni, lakini mbona tunanyanyaswa na hatupati haki yetu ya kikatiba”? Namshukuru Mhe. Nzambia, Mjumbe wa Kilome kwa kuleta Hoja hii Bungeni. Naunga Hoja hii mkono mia kwa mia ya kuwatetea wazee wetu ambao wametuzaa. Tukijiangalia hatungekuwa hapa kama si wale wazee ambao walituzaa kule nyanjani tulikotoka. Tunawapatia heshima kuu na kuwatetea. Naomba Bunge hili liweze kuwasaidia kwa kupitisha Hoja hii ili waongezewe zile pesa zao. Pia, idadi yao iongezewe kwa sababu tangu mradi huu uanzishwe mwaka wa 2016 walisimamisha uongezaji wa watu wengine. Basi Bunge hili liweze kupitisha na kuunga mkono wale wazee waongezwe katika ile orodha. Pili, zile pesa ni finyu sana. Kule kwetu tunasema ni pesa za wazee kununua tumbaku peke yake kwa sababu hawawezi kujikimu kimaisha ilhali, wamezaa watu ambao wanaheshimika, ni wazima na wao wamepoteza nguvu zao. Mimi ninatoka sehemu ya Kwale ambayo ina maeneo Bunge manne; Lungalunga, Msambweni, Matuga na Kinango. Zile sehemu zina wazee wanyonge zaidi na itabidi mzee atembee au atumie njia ya usafiri kama bodaboda ndio afike katika kituo cha kulipia hizi pesa. Wengine wanatumia hata siku tatu ndio wazipate zile pesa. Wakifika katika mabenki yale, mzee anakaa siku mbili kwenye baridi akisubiri. Ningeomba zile huduma zishukishwe kule nyanjani, ili tusimpate mzee ametoka Kinango kuja kuzichukua pesa zile pale Kwale ambapo ni County Headquarters, akiwa ametoka takriban kilomita mia mbili ama mia tatu. Hiyo ni hujuma. Tunawasaidia lakini pia tunawanyanyasa kwa njia moja au nyingine. Mzee amekaa kwa baridi siku mbili kungoja shilingi elfu mbili. Jambo lingine ni, wale ndugu zetu wanaowachukulia wale wazee zile pesa, ningependa pia wawatendee haki, kwa sababu sisi kama jamii ya Wapwani au jamii ya Kiislamu, tunaamini kuwa dhuluma ni kitu kibaya. Wewe umemleta mzee aliye mnyonge na maskini, labda haelewi anapokea pesa ngapi, halafu wewe unazichukua zile pesa kitita fulani na kutia mfukoni. Serikali lazima itafute njia nzuri na mbadala ya wale wazee kufaidika wao wenyewe directly . The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}