GET /api/v0.1/hansard/entries/1218149/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218149,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218149/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
"speaker": null,
"content": "Nilikutana na wazee ambao walikuwa wamekuja sehemu ile kuchukua pesa. Unapata mzee anafanyishwa ile nenda-rudi, kwa sababu ya hizi alama za vidole. Wakati mwingi mtu akifika umri fulani, hizi alama za vidole ambazo kwa lugha ya Kingereza zinaitwa finger prints, zinapotea. Unapata mzee anaambiwa hawezi pewa pesa kwa sababu finger prints zake zimepotea. Yule mzee anataabika na kukaa kwenye jua au baridi siku mbili ama tatu, na pengine pia asipate zile pesa, arudi nyumbani halafu arudi pale tena baada ya miezi sita. Kama tunawasaidia wazee hawa, basi pia haki itendeke na tuweze kuwafanyia njia nyepesi ya kuweza kufaidika na pesa zile."
}