GET /api/v0.1/hansard/entries/1218150/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218150,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218150/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Fatuma Masito",
    "speaker": null,
    "content": "Jambo lingine ambalo ningependa kuongezea ili kuongeza chumvi au kuongeza uzito wa Hoja hii iliyoletwa na Mheshimiwa wa kutoka Kilome, Mhe. Nzambia, ni kuwa katika Bunge hili, taifa hili letu na Serikali hii tuliyonayo, tuwafikirie wale wazee wetu kuweza kupata bima ya afya. Wazee wengi ni wajane na sisi tunajifahamu katika jamii mara nyingi wazee wale huwa wameachiliwa, hawaangaliwi, hawashughulikiwi, hakuna mtu anayewajali na pia kupata matibabu ni shida."
}