GET /api/v0.1/hansard/entries/1218153/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218153,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218153/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "speech",
"speaker_name": "Marsabit County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Naomi Waqo",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nashukuru Mhe. Nzambia aliyeleta Hoja hii ambayo ni ya kutusaidia na pia kuwasaidia wazee mahali tunapotoka. Ninaiunga mkono Hoja hii kwa sababu ni ya maana na tukiipitisha inaweza kuwasaidia wale watu wanaotuombea na kutuunga mkono kutoka kule chini. Tunavyojua, sisi Waafrika ni watu ambao tumekuwa tukiwaangalia wenzetu na tunapenda kuangaliana. Lakini hivi sasa hiyo hali ya kuchunga na kusaidiana imeisha ndani ya watu. Vijana na wasichana wala watoto hawakumbuki kutunza wazazi wao vile tulikuwa tunafanya hapo awali kama Waafrika. Hii ni kumaanisha kuwa hii culture ambayo tumepoteza inaendelea kutuathiri na hiyo ndiyo inafanya wazee wetu kuumia kwa njia mbali mbali katika uzee wao."
}