GET /api/v0.1/hansard/entries/1218155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218155,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218155/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Marsabit County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Naomi Waqo",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa mambo ya kuhakikisha kwamba wale ambao wamefikisha miaka sitini ama sitini na tano wamesajiliwa na wameangaliwa vizuri ni muhimu. Wakati wa campaign nakumbuka nilitembea maeneo mbali mbali na wazee wengi hawakua wamesajiliwa kama watu wanaofaa kuhudumiwa na kupata hiyo pesa. Hata katika kusajiliwa wanaohusika kama machifu na wazee wa kijiji wanaosimamia hayo mambo, wanafaa kuangalia kwa makini ni kina nani wanaofaa kupata pesa zile. Hata kama tunasema kwamba wazee wote wana haki ya kupata, kati ya hao wazee kuna wale ambao ni disabled, hawajiwezi na wanahitaji kupewa nafasi ya kwanza ili waweze kupata nafasi na wahudumiwe kwa njia ya karibu sana. Kati ya hao wazee pia kuna wale ambao wako kwa hali ya umaskini zaidi. Kwa hivyo, hata kama tunasema wazee wote ambao wamefikisha miaka sitini na sitini na tano waangaliwe, tunafaa pia kuangalia kati ya hao, ni nani aliye maskini zaidi, nani asiyejiweza kabisa na ni nani aliye na shida ambayo pia sisi hatutaweza kusema kwa sababu wengine wako na shida za afya kama blood pressure, shida ya sukari inayopanda na kuwasumbua, na wengine wana shida zinazohitaji matibabu. Kwa hivyo, hata tukipendekeza wapate usaidizi huu, mambo ya afya yao inafaa kuangaliwa na waweze kupata huduma ya karibu hasa wale ambao wanaumia kwa njia mbali mbali."
}