GET /api/v0.1/hansard/entries/1218160/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218160,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218160/?format=api",
"text_counter": 247,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, PAA",
"speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": " Kwanza, nashukuru Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Baada ya kupewa likizo na wananchi 2017, ilipofika 2022, waliona kwamba hili Bunge linakosa wazee. Ndio maana wakaniregesha katika Bunge hili. Hii Hoja inahusiana na wazee. Kwa hivyo, nashukuru na kutambua Mhe. Nzambia kwa sababu ya kuleta hii Hoja, kwa sababu ni ya muhimu sana katika Bunge na Jamhuri nzima. Kuwakumbuka wazee ni kama kuikumbuka kale yetu."
}