GET /api/v0.1/hansard/entries/1218161/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218161,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218161/?format=api",
    "text_counter": 248,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
    "speaker": null,
    "content": "Hoja hii tunaizungumzia kwa sababu usajili ulikomeshwa karibu miaka saba iliyopita. Hadi sasa, mambo mengi yamepita. Ushuhuda ambao nilishuhudia wakati nilipokuwa likizoni ni kwamba hawa wazee wanastahili kupewa heshima. Tuna taifa sasa kwa sababu ya hawa wazee. Lakini hali wanayoishi na kuchukuliwa ni kama ni watu waliolaaniwa. Eneo Bunge ninalotoka la Kinango ni sehemu kame. Hali ya wazee inazidi kudorora zaidi kwa sababu hali si hali. Niko hapa Bungeni lakini karibu kila siku, nakutana na maombi ambayo yanawasilishwa kwa njia ya simu kwamba kumekuja wazee lakini hawajakula kwa zaidi ya siku tatu. Umri wao ni ule umezidi miaka sitini na tano na kuendelea. Sasa ukiangalia, kweli kama taifa tunaweza kusema tunaendelea lakini kama jamii ile imewachwa nyuma, huwa ni mateso makubwa sana. Kufaulu kwetu kama jamii ni kuwakumbuka hawa wazee wetu na kujua kwamba ni watu ambao wanastahili kutunzwa. Kutoka mwisho wa usajili ambapo ni miaka saba iliyopita, pesa tunazowapatia na ule utaratibu unaofuata, wakati mwingine inakuwa kama ndoto kwa sababu unasajiliwa mpaka wakati mwingine unakumbana na mauti ndio pesa zinaingia. Wakati mwingine wale tunawaorodhesha kama next of kin, tunapowatuma kwenda kuwasaidia wazee hawa, wao pia wanatumia ufisadi na kuwalangua wazee hawa. Anapelekwa kwa benki na akifika hapo, anaambiwa atie sahihi . Akirudi, anaambiwa pesa zimekosekana lakini zimetoka."
}