GET /api/v0.1/hansard/entries/1218162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218162/?format=api",
    "text_counter": 249,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kinango, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
    "speaker": null,
    "content": "Nakumbuka dhahiri kwamba wakati mmoja, kulikuwa na mzee kule Pwani ambaye alikuwa amefanya kazi Halmashauri ya Bandari ya Kenya zaidi ya miaka 30. Alienda kustaafu na pesa yake ilikuwa inaingia kwa Benki ya Barclays. Kila akienda benki, alienda na kijana ili aende akatolewe pesa. Jambo lililokuja kudhihirika baadaye ni kwamba kijana alikuwa akimpeleka mzazi kwa benki na akifika anamjazia form ya kutoa pesa na baadaye anamwambia pesa hazijaingia. Pesa zilipokwisha, ikabidi mzee atafute msaada wa Mjumbe ili apate kujua kwa nini pesa zake zimechelewa. Tulipokuja kuuliza swala katika Bunge hili, tukapata Ripoti kutoka kwa Halmashauri ya Bandari kwamba pesa zilikuwa zimeingia benki."
}