GET /api/v0.1/hansard/entries/1218164/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218164,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218164/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kinango, PAA",
"speaker_title": "Hon. Gonzi Rai",
"speaker": null,
"content": "Tunapoenda kusajili watu kwa sababu ya kura, wakati mwingi, kuna utaratibu unaotumika ili watu wote wakate kura. Usajili wa wazee wetu unastahili kufanyika kwa utaratibu fulani kuhakikisha kuwa wanasajiliwa vilivyo. Kufikia sasa, idadi ya wale wanafaidika na pesa za uzeeni ni wachache kuliko wale hawajasajiliwa. Kilio na masikitiko yao tunayazingizia kutokana na climate change nchini. Hakuna mvua na kwa hivyo, ardhi haimei chakula kwa sababu ya laana ya watu tuliowatesa. Mhe. Spika wa Muda, aliyoyafanya Mhe. Nzambia ni dhahiri kuwa alijua kuwa wazee wetu wanateseka. Tulizungumzie hili swala na baadaye, tulipitisha ili lipate utaratibu mwafaka wa kuhakikisha kuwa hizi pesa zimepatikana na kuwe na utaratibu mwafaka wa usajili utakaowawezesha wazee wetu wapate pesa zao baada ya muda fulani ama msimu fulani. Ingekuwa bora iwapo tayari, zingekuwa zimetoka na tayari ziko kwenye benki zao. Hakuna dhambi kuweka orodha ya majina ili kuhakikisha kuwa anayeenda katika benki yuko na uhakika kuwa pesa ziko kuliko mtu afunge safari kutoka Kinango mpaka Mariakani, Kinango mpaka Kwale na atakapofika, hakuna pesa. Pesa anazotumia baada ya safari, zinazidi pesa alizolipwa. Swala hili linauma. Ninamshukuru na niko na matumaini kuwa heko na sifa zitamfikia Mjumbe husika, Mhe. Nzambia kwa sababu Hoja nyingi zimeletwa katika Jumba hili lakini hii ni muhimu sana. Ninakushukuru Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ili ieleweke kuwa hii ni Hoja ya maana sana hasa siku ya leo. Mhe. Spika wa Muda, Mungu akubariki na tuendelee kupeleka Bunge letu mbele. Asante."
}