GET /api/v0.1/hansard/entries/1218362/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218362,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218362/?format=api",
"text_counter": 170,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, makadamia ni mengi katika maeneo ya Manyatta na Runyejes, Kaunti ya Embu. Watu wengi hupanda makadamia kwa wingi kwa sababu hapo ndipo tunapata hela nyingi. Kwa hivyo ninaunga mkono ya kwamba tuangalie jinsi ambavyo tutafanya, ndio mkulima afaidike. Sasa hivi, bei ya makadamia iko chini sana ukilinganisha na hapo zamani ambao tulikuwa tunapata wanunuzi kutoka nje. Wakati huo, kilo moja ilikuwa zaidi ya shilingi 100. Sasa hivi, kilo moja ni takribani shilingi 30 au 40. Wanunuzi wa kigeni walikuwa wananunua makadamia yetu moja kwa moja kutoka kwa mkulima. Hapo ndipo matajari wa Kenya walitoa pesa nyingi na kuzuia wanunuzi wa kigeni. Hilo ndilo lilisababisha shida. Kwa hivyo, ninaunga mkono. Hivyo vizingiti viondolewe ndio soko liwe huru ili kila mkulima auze vile anataka. Pia, watu kutoka nje wakubaliwe kuja Kenya kununua hayo makadamia. Ninaunga mkono."
}