GET /api/v0.1/hansard/entries/1218363/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218363,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218363/?format=api",
    "text_counter": 171,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "a: Asante, Bw. Spika. Ni vizuri ukweli usemwe. Kulingana na hiyo taarifa kuhusu karanga, utapata ya kwamba sio karanga peke yake bali ni mazao yote hapa nchini Kenya. Tutilie ukulima manani inavyofaa. Tunaongea kuhusu mazao ya biashara peke yake kwa mfano, pareto mengine. Hatujatilia mkazo mazao ambayo yanaweza kutumika hapa nyumbani. Utasikia tukisema kuhusu mpunga au mahindi lakini si mimea ile mingine kama vile karanga, korosho na viazi kule Nyandarua. Haya hatuyatilii maanani kama Serikali. Tunapaswa kuyatilia maanani kwasababu yatatusaidia. Sisi, kama Serikali ya Kenya Kwanza, tumesema tutaagiza vyakula kutoka nchi za nje ili watu wetu wasikose vyakula. Hii itawezekana ikiwa tutatilia maanani ukulima. Kulingana na ile Taarifa ingine iliyotajwa, kulisemekana mazingira yetu yameharibika sana. Kulisemekana ni mpaka njia mbadala itafutwe ya kuyalinda. Juzi tu, kuna Taarifa iliyoletwa katika Seneti kuhusu miti ya mibuyu ambayo watu wanaambiwa waangalie mazingira wanapoikata. Hata ukiwaeleza watu watunze mazingara, unafaa uwaambie baada ya kuchunga hii miti watasaidika vipi. Hii ni kwa sababu wanategemea ile miti na wanalipwa pesa wakiikata."
}