GET /api/v0.1/hansard/entries/1218379/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218379,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218379/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chute",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13583,
"legal_name": "Chute Mohamed Said",
"slug": "chute-mohamed-said"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Mahali nimetoka, hatuna korosho, makadamia ama vitu kama hivyo. Nitafurahi sana akinifunza. Sen. Kinyua akiniuliza maneno ya nyama, nitamwambia hiyo ni ya ngamia au mbuzi kwa kunusa tu bila kuonja. Sen. Ali Roba ni shahidi wangu hapo. Ninashukuru amenieleza. Bw. Spika, shida tuliyo nayo - ukiangalia upandaji wa korosho na makadamia - ni kwamba ukulima umekuwa na shida sana. Mashamba za kahawa zote zimebadilishwa kuwa biashara za nyumba. Kahawa na majani chai zinaendelea kupotea. Ile shida tuko nayo ni kwamba wakati huu maziwa tunayotumia yanatoka Uganda. Kwanza, maziwa haya yanatoka Uropa na kupelekwa Kampala yakiwa maziwa unga. Huko Kampala wanaongeza maji na wanaleta hapa kama maziwa ya Uganda. Sasa ukulima wetu, si nimesema umezikwa? Kamati inayohusika na mambo hayo ni lazima iaangazie mambo hayo vizuri na hatua kali zichukuliwe. Asante."
}