GET /api/v0.1/hansard/entries/1218769/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218769,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218769/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "speech",
"speaker_name": "Elgeyo Marakwet County, Independent",
"speaker_title": "Hon. Caroline Ng’elechei",
"speaker": null,
"content": ". Nitaongea hivi ili watu wangu wa Elgeyo Marakwet waelewe nitakachochangia. Naunga mkono dada yangu Cecilia kutoka Kaunti ya Turkana. Huu wizi wa mifugo katika bonde la Kerio umeleta maafa mengi. Kwa mfano, mwaka huu Elgeyo Marakwet, tangu Januari tarehe ishirini watu zaidi ya ishirini wamezikwa wakiwemo watoto, akina mama na hata wakongwe. Ni aibu tunapoendelea kuliongelea janga hili kwa sababu dunia imeendelea. Watu hawauwani na kunyang’anyana mifugo – emaciated animals tena. Watu sasa hivi wanaongea maneno ya climate change, technology, cybercrime na vitu vingine ambavyo vinaendelea katika dunia. Sisi bado tunalia sana. Mimi ni Women Representative wa Elgeyo Marakwet County. Tuko na baraka Kaunti ya Elgeyo Marakwet. Ardhi yetu ni nzuri na inaweza kuzalisha mazao ya kutulisha. Lakini kila kuchao, nikutanapo na Rais mimi humwomba atusaidie na relief food. Sababu ni kuwa kwa miaka mitano iloyopita, watu wa bonde la Kerio hawajaweza kupanda na kuvuna kwa kuwa majangili huwa wana cross River Kerio na kuwavamia wanapo fanya kazi zao. Wakati mwingine, majangili ambao wamemea pembe hungoja watu wapande watermelon na nyanya kisha walete mifugo yao. Mara nyingi wanapokuja kulisha mifugo yao mimi huwauliza kwa nini wanachunga mifugo na bunduki na wao husema ng’ombe hawawezi kuchungwa na fimbo. Sisi tunasononeka Elgeyo Marakwet. Kuna shule ambazo hazina wanafunzi. Mfano ni shule ya upili ya Kerio Valley. Wanafunzi walihama kwa sababu ya shida ya insecurity . Sasa hivi tunavyo ongea, watu wengi wamekuwa wagonjwa wa akili kutokana na mawazo. Huwezi kushinda ukiwaza kama Mkenya wa kawaida ilhali hujui ni kipi kitakufanyikia wewe na watoto wako kesho. Mara nyingi tunaongea kuhusu vijana kuandikwa kazi. Vijana wa Kerio hawajapata nafasi ya kuja Nairobi kuhustle kwa sababu wanahofia kuwa watakapo toka makwao, majangili wataenda kuwavamia mama zao, mabibi zao na watoto. Kwa hivyo, wamebaki makwao ili wawaangalie wakingoja wanalolijua. Haya manaeno tumeyaongea sana na wakati mwingine hakuna goodwill ama ari ya kuhakikisha kwamba hili jambo limeisha. Juzi nilimsikia Mbunge wa Sigor, Lochakapong, akiuliza wale ng’ombe waliouwawa na polisi watafidiwa lini. Heri yeye. Sisi ni nani ataturudishia maisha ya binadamu? Kwake, ng’ombe ni muhimu kuliko maisha ya wasichana wadogo na mzee mkongwe waliouwawa juzi. Yeye anaweza kusimama Bungeni kutaka fidia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}