GET /api/v0.1/hansard/entries/1218770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218770,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218770/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Elgeyo Marakwet County, Independent",
"speaker_title": "Hon. Caroline Ng’elechei",
"speaker": null,
"content": "ya ng’ombe ambao hawakuwa na afya. Ni ng’ombe ambao hata mimi naweza fidia. Hiyo ina maana kuwa ubinadamu umewatoka wengine wetu. Mara nyingi Mhe. wa Baringo, Jematiah apigapo kelele mimi humuelewa kwa sababu sisi hulia mara nyingi. Ni uchungu kumwona mtu akihama kwake. Wanakoishi watu Tiaty na Sigor hakuna nyasi. Watu wa Elgeyo Marakwet hawafugi kwao kwa sababu hakuna lishe ya mifugo. Wao ndio huja kwa ardhi yetu na kutusongesha. Tuwaulizapo, wao hutupiga risasi. Serikali iangalie swala hili. Sisi ni Wakenya kama Wakenya wengine. Tuna haki ya kuishi kama wengine. Hatutaendelea kimasomo hata tukipewa free secondary education, free barabara na free maji ikiwa hakutakuwa na security . Hali hii imefika kiwango ambacho sisi tutaomba tuhamishwe na tupelekwe kwa kambi ya wakimbizi ili tuwe wakimbizi kwa ardhi yetu. Hatuwezi tolerate any more . Imekuwa uchungu sana."
}