GET /api/v0.1/hansard/entries/1218782/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218782,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218782/?format=api",
"text_counter": 307,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kapenguria, UDA",
"speaker_title": "Hon. Samwel Chumel",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Nimesikia yale wenzangu wamesema hapa na ninataka niwaeleze jambo. Wengine wetu tulikuwa tunaongea mnavyoongea hapa tukifikiri italeta faida na eti watu wakikuona, wanakupigia makofi. Ukweli ni kwamba kesho bado wataumia. Nataka tuunge mkono yale Mjumbe wa Kuria amesema. Ninatoka Kapenguria. Tulikuwa tunapigana upande wa Trans Nzoia, Uganda, Marakwet na Turkana lakini kwa sasa hutasikia watu kutoka maeneo hayo, haswa Kapenguria Kaskazini, wakipigana. Tulikuwa na clashes mwaka wa 1992 tulipoanza multipartism lakini ile vita ingine yote kuanzia mwaka wa 1997 mpaka ile yenu iliyokuwa kubwa zaidi haikuingia kwetu. Hii ni kwa sababu tuliketi chini na tukaongea. Marehemu Rais Moi alileta kitu kilichokuwa kinaitwa Operesheni Nyundo. Mhe. Nkaiserry ndiye aliyeongoza operesheni hiyo. Marehemu Kibaki akakuja na yake iliyoitwa Operesheni Dumisha Amani . Wale wanajeshi waliokuwa wanagonga watu nyundo ndio walikuwa wanakaa chini na watu kuwauliza shida ni gani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}