GET /api/v0.1/hansard/entries/1218783/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218783,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218783/?format=api",
"text_counter": 308,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kapenguria, UDA",
"speaker_title": "Hon. Samwel Chumel",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, umesikia kwamba hiyo sehemu ni ile iliyokuwa wilaya ya kitambo . Hata wale wamishonari waliokuja kutusaidia kiroho walitoka Uganda. Walipitia mahali panaitwa Modat kuja kwetu. Walichukua muda kabla ya kufika kwenye Kanisa la Kikatoliki. Walifika mahali panaitwa Tartar kwanza. Hii leo, mahali hapo ni shule ya wasichana ya kitaifa. Haya yote ni kwa sababu ya kanisa. Wafuata dini waprotestanti wa kanisa la Kianglikana wakapitia Uganda mahali panaitwa Nasokol. Kwa sasa kuna shule ya upili mahali hapo na neno la Mungu linaendelea. Kwa ile hali ya watu kuchangana, Marehemu Rais. Kibaki alikuja akawauliza ni ipi shida yao. Wanajeshi ndio waliketi chini na watu. Waliwauliza kilichokuwa kinawasumbua hadi kufikia kuvamia Trans Nzoia. Natumai kuna watu kutoka Trans Nzoia walioshuhudia. Walipoulizwa, walisema kuwa maji ndio chanzo kikuu cha vurugu. Wakati wa kiangazi, iliwalazimu kuingia Trans Nzoia. Hapo ndipo wahandisi wanajeshi walitumwa kuchimba maji pale. Aidha walijengea watu barabara na hema kubwa zilizotumika kama hospitali za kutibia wananchi. Matendo hayo yalileta uhusiano mwema kati ya jamii zilizokuwa zikipigana awali ikawa wanajeshi wamewaweza. Haya yote yaliwaleta watu karibu. Watu kutoka West Pokot hawakuwa na sababu ya kwenda Trans Nzoia kwa sababu maji na barabara vilikuwa vinapatikana pande zote. Isitoshe, hospitali zilikuwa zimeanza kujengwa. Namshukuru Rais wa sasa hivi. Wakati alikuwa Naibu wa Rais alituita sote kama jamii ya North Rift na tukawa na Peace Caravan. Aliyekuwa Inspector General (IG) wakati huo, Bw. Joseph Boinett aliungana nasi pamoja na askari wake. Tulizunguka mkutano mmoja hadi mwingine tukiongea kuhusu amani. Ni juzi tu ndiyo hiyo Peace Caravan ilianguka kwa sababu watu wapya, wasioelewa shida ilikuwa wapi, waliingililia. Utapata mtu akiongea hapa akifikiri atajulikana na mambo anayosema yatafanyika. Acha tuketi chini! Ninashukuru hii Serikali maana imesema wanajeshi hawatatoka mahali hapo mpaka wafanye maendeleo. Ukiangalia eneo la Baringo… Ninataka waketi chini ili waone ni nani alisababisha Tiaty iwe ilivyo. Maendeleo kama vile barabara ya lami, masomo, na stima yanapelekwa hadi mahali panaitwa Loruk kisha yanakomea hapo. Wamejenga kanisa la African Inland Church (AIC) hapo. Mimi pamoja na aliyekuwa Rais Moi, tulikuwa washirika wa kanisa hilo. Upande wa chini hakuna kanisa. Ninamshukuru marehemu Rais Kibaki kwa sababu ni wakati wa utawala wake ndiyo barabara za lami, na shule zilijengwa. Jeshi lilifika huko ndani wakati marehemu Michuki alikuwa Waziri. Hatutaki kurudi huko nyuma. Kapenguria hatuna shida. Ni eneo ambalo ni"
}