GET /api/v0.1/hansard/entries/1218813/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1218813,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218813/?format=api",
    "text_counter": 338,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Magarini, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, hakuchi hakuchi hucha. Ama kwa kusema kweli, suala hili la usalama ni tata sana, lakini yapaswa tufahamu kwamba usalama huanza na mimi na wewe. Vile tutakavyo ishi ndivyo itakavyochangia usalama wetu. Sehemu hizi husika katika mjadala huu zina historia ya wizi wa ng’ombe kwa miaka na mikaka. Imekuwa kama mchezo kwao. Huyu akimwibia huyu leo, kesho yake ni yule mwingine atakayeibia mwenzake. Haya yote yamechangiwa na kuachwa nyuma kimaenedeo. Nilipata nafasi ya kutembelea Turkana, pale Kapenguria. Niseme hivi: kwangu kuna barabara mbaya, lakini vile nilivyoona katika sehemu hii, barabara ni mbaya zaidi. Hii inaweza kuchangia kutokuwa na usalama. Barabara na vituo vya polisi, ambavyo sikumbuki vikiwa njiani hadi nilipofika Turkwel, viko hali mbaya. Hali ni ya kuhangaika kwa kuingia kwa shimo na kuamka. Hali ilikuwa mbaya. Ukitazama runinga uone hali ilivyo kuhusu janga la njaa katika maeneo hayo, hata kama wewe sio mkaazi wa Turkana, utatokwa na chozi kwa sababu ya yale utakayoyaona. Hii ni ishara kwamba ndugu zetu wameachwa nyuma. Inahuzunisha maana Kenya ni moja. Inastahili kwa sasa niipongeze Serikali kwa ile hatua ambayo imechukua lakini pia niseme haijatosha. Hawa ndugu zetu wanastahili kuongezewa vituo vya polisi. Kama kituo kimoja kitakuwa mbali na kingine iwe ni kilomita tano au kumi ikizidi. Ilivyo wakati huu, unatembea zaidi ya kilomita ishirini na tano au hamsini lakini huoni ofisi ya Serikali. Jambo hilo halitaleta usalama katika maeneo haya. Ndugu zetu wako mipakani. Wakati mwingi ambapo operesheni inaendelea, wale majangili hawako hapa nchini. Wamevuka mipaka kwenda kuficha silaha. Wakirudi huku, huwa wana mikono mitupu. Hiyo tayari ni shida. Laiti mipaka yetu ingelindwa kisawasawa, ndugu zetu wangekuwa na hali nzuri ya usalama na wangejiendeleza."
}