GET /api/v0.1/hansard/entries/1218829/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218829,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218829/?format=api",
"text_counter": 354,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sotik, UDA",
"speaker_title": "Hon. Francis Sigei",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia mjadala ambao ni wa maana sana. Nashukuru mwakilishi wa Turkana kwa kuleta mjadala huu. Nauunga mkono. Pili, naunga mkono Serikali hasa Wizara husika kwa yale wanayofanya upande wa North Rift. Tungependa kuona Waziri, Prof. Kindiki, akichukua hatua ya kuunganisha watu. Tungependa kuona viongozi wote wa North Rift wakifungiwa kwa nyumba na viongozi wa dini ili wazungumzie vita hivi. Tatu, nakemea mauaji yanayoendelea huko. Tumepoteza watoto, machifu na askari. Kuna umaskini. Shule zimefungwa. Haya mambo yataendelea hadi lini? Naomba Serikali kutuma wanajeshi. Kuna wanajeshi Garissa, Mandera, na Wajir. Tungependa kuwa na vituo vya wanajeshi Turkana ili watu wafanye kazi na wanafunzi warudi shule. Mhe. Spika wa Muda, ningeomba barabara zitengenezwe katika hizi sehemu. Wenyeji wa maeneo hayo pia wapewe maji, stima, na wejengewe shule nzuri. Serikali lazima iweke pesa katika maeneo hayo."
}