GET /api/v0.1/hansard/entries/1218837/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218837,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218837/?format=api",
"text_counter": 362,
"type": "speech",
"speaker_name": "Baringo South, UDA",
"speaker_title": "Hon. Charles Kamuren",
"speaker": null,
"content": "Pili, ninatambua kazi ambayo Waziri Prof. Kindiki anafanya pamoja na Wizara yake ya kujaribu kuhakikisha kwamba usalama unapatikana. Katika Eneo Bunge langu la Baringo Kusini, Mochongoi na Mukutani ni sehemu ambazo zilikua gazetted ilhali operesheni hiyo haijafika. Ninapozungumza, mbuzi waliibwa na sauti za risasi zilisikika maeneo hayo masaa ya saa tisa usiku. Watu walihangaishwa sana na mbuzi wakachukuliwa. Wiki iliyopita vile vile, waliibiwa upande wa Lomaiwe. Hatujapata usaidizi vile tulivyotarajia. Tuko na imani kwamba kuna mpangilio unaofuatwa. Ninaomba wale wanahusika waharakishe ili wasaidie watu pale."
}