GET /api/v0.1/hansard/entries/1218839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1218839,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1218839/?format=api",
"text_counter": 364,
"type": "speech",
"speaker_name": "Baringo South, UDA",
"speaker_title": "Hon. Charles Kamuren",
"speaker": null,
"content": "wengi. Isitoshe, shule tano hazijafunguliwa hadi leo. Tuko na nini sisi? Ninaomba watu wasaidiwe. Mambo ya upokonyaji silaha yaendelezwe. Mhe. Spika, nimeshangaa kusikia Mbunge mmoja akisema kuwa watu wake wakae na bunduki. Bunduki ni haramu. Bunduki ni ya askari wa Kenya. Hatutaweza kuongea juu ya amani wakati watu wako wana bunduki. Katiba inasema kuwa bunduki ni ya askari. Raia wote wameamrishwa na Serikali kutoa bunduki. Ikiwa watakataa, basi sharti Serikali itumie nguvu kutoa bunduki hizo. Nimeshangazwa hata na Wabunge wengine ambao wanauliza juu ya wanajeshi. Je, wanajeshi wamefanya makosa gani? Hawajakuja kufanya kazi bali kusaidia polisi. Hii imekuwa biashara lakini ninaona Wabunge wenzangu hawataki kusema ni biashara ya watu fulani ndiposa wanahangaisha watu. Ningependa kusema kuwa bunduki ichukuliwe kutoka kwa raia na watu wapewe National Police Reserve. Magaidi wote wanaohusika, hata kama ni Wabunge wakamatwe. Bunduki zote haramu zirudishiwe Serikali. Hao magaidi wasibembelezwe. Ugaidi ni ugaidi. Hata watu wangu hawana maendeleo. Kwani ni lazima watu wako wachukue bunduki ndiyo Serikali ilete maendeleo? Yaani wanatisha Serikali na bunduki ndiyo watengenezewe barabara na shule. Ni sharti watoe bunduki ndiyo Serikali ilete maendeleo. Kama kiongozi, ugaidi wa kuambia watu wakae na bunduki ndiyo Serikali iwasaidie…"
}