GET /api/v0.1/hansard/entries/1219236/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219236,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219236/?format=api",
    "text_counter": 102,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ganze, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Naibu Spika, kwa kunipatia nafasi kuchangia Hoja hii. Kabla nichangie, ningependa nijiunge na viongozi wenzangu kuwatakia akina mama wa nchi yetu siku njema wanaposherehekea siku ya wanawake ulimwenguni. Nikirudi kwa mada, ningependa kumpongeza Mhe. Nzambia kwa kuleta Hoja hii. Kusema kweli, wazee humu nchini Kenya wamepata shida kwa sababu wengi wao hawapati hizi pesa za uzeeni. Imekuwa kitambo sana tangu mwaka wa 2016 Serikali iandikishe wazee. Kutoka mwaka huo hadi sasa, tuko na wazee wengi ambao wamefikisha miaka ya kuandikishwa lakini hawapati pesa. Kwa hivyo, ningependa kusema kuwa ni vizuri Hoja hii imeletwa kwa wakati ufaao. Wazee wote waandikishwe ili waweze kupata hata kama ni pesa kidogo lakini zinawasaidia kwa mahitaji yao."
}