GET /api/v0.1/hansard/entries/1219246/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219246,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219246/?format=api",
"text_counter": 112,
"type": "speech",
"speaker_name": "Rabai, PAA",
"speaker_title": "Hon. Kenga Mupe",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu wa Spika. Ninaunga mkono Hoja hii kuhusu namna wazee wanaweza kulipwa. Ninampongeza Mhe. Nzambia kwa kuileta Hoja hii wakati unaofaa. Kwa hakika, kuna wazee vijijini ambao hali yao ya kimaisha na kiafya siyo nzuri. Hii Hoja ikipita, nina uhakika kwamba wataweza kupata fedha ambazo zitawakimu kimaisha. Sheria inasema kwamba mzee anaweza kupata fedha hizi akihitimu miaka sabini. Ninaomba Bunge hili liweze kupunguza ile miaka kwa sababu wazee vijijini wanakufa kabla ya kufikia miaka sabini."
}