GET /api/v0.1/hansard/entries/1219370/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219370,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219370/?format=api",
    "text_counter": 236,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo imeletwa kwenye Bunge hili na Mjumbe wetu wa Dagoretti North, Mhe. Beatrice Elachi. Ni Hoja muhimu sana kwa sababu mambo tunayoyazungumzia leo yanahusu ujenzi wa nchi yetu kwa kutumia rasilimali inayopatikana katika nchi yetu ya Kenya. Kabla sijaendelea kuchangia huu mjadala, nachukua nafasi hii kuwapongeza akina mama wote ndani ya Bunge hili la kitaifa. Pia, nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Elachi kwa kuleta Hoja hii. Ninakumbuka vizuri vile tulivyoteuliwa pamoja kwenye Bunge la Seneti. Tulikuwa pia pamoja na Mhe. Martha, na nawapa pongezi sana. Mungu awasaidie sana. Ninachukua nafasi hii pia kuwapongeza akina mama wote tukianza na wazazi wetu ambao walituzaa, kutulea na kutupa nafasi ya kusoma. Hoja hii ya leo ni ya kujenga uchumi wetu. Bila kuzungumza mambo mengi, ningependa kuzungumzia Nakuru. Nakuru imejulikana kwa sekta ya ufugaji wa kondoo. Mnaelewa kuwa kondoo wa Nakuru ni wa hali ya juu na wana thamani ya juu. Hatuna haja ya kununua zulia kwenye maduka makubwa. Nahisi kuwa hii ni nafasi nzuri kwa wakulima The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}