GET /api/v0.1/hansard/entries/1219371/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219371,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219371/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": "kujenga uchumi wao. Nina imani kuwa Hoja hii ambayo imeletwa kwenye Bunge La Kitaifa itaweka mambo ya utekelezi kipaumbele. Hakuna haja ya kuongea mambo mengi bila utekelezaji. Ninamuomba Mhe. Elachi ahakikishe kuwa itatekelezwa. Hoja hii inaenda sambamba na yale mambo yote akina mama wanafanya pale mashinani. Nawakumbuka akina mama kutoka upande wa Kuresoi South, Kuresoi North na Elburgon. Wanashona sweta za watoto na watu wazima. Wanatengeneza pia zulia ambazo zinatumika kufunika miguu ili kuzuia baridi. Zile mashine ambazo wanazitumia zimetengenezwa kule nyumbani. Kwa hivyo, tukihakikisha kuwa Hoja hii imetekelezwa, basi akina mama hawa watapata mashine na chochote wanachohitaji kuendeleza kazi zao za mkono. Vile vile, itasaidia wale akina mama ambao hawajaenda shule. Kuna akina mama ambao hawakupata nafasi ya kusoma lakini wana utaalamu fulani maishani. Ninajua kuwa Hoja hii ikitekelezwa, kila mama atafaidika na hivyo tutaboresha uchumi nchini Kenya. Ni jambo la kushangaza kuona Mkenya akifurahia bidhaa kama nguo kutoka nje ya nchi. Huwa ninaona watu wakifurahia kusema kuwa bidhaa kama shuka inatoka Misri ama sweta imetoka Uturuki…"
}