GET /api/v0.1/hansard/entries/1219404/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219404,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219404/?format=api",
    "text_counter": 26,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Nashukuru, Bw. Spika, kwa fursa hii umenipa ili nichangie hili ombi ambalo limeletwa na mhusika. Kwanza kabisa niseme ya kwamba, ni haki ya kila Mkenya kuleta ombi katika Seneti. Ningependa kusema ya kwamba nashukuru kwa sababu hili swala la malipo ya walimu ambao walistaafu limechukua muda mrefu sana. Mwaka wa 1997 walimu wa Kenya waligoma. Serikali ya Rais aliyekuwemo, Mhe. Marehemu Moi, aliwapa nyongesa ya mshahara lakini ile Serikali haikutimiza kulipa wale walimu. Mwaka wa 2002 wakati uongozi ulikuja mpya wa Mhe. Marehemu Rais Kibaki, iliamua kulipa wale walimu malipo yao ya nyongeza ya mishahara. Lakini kuna walimu kati ya 1997 na 2002 walikuwa wamestaafu kabla ya kupata malipo yao ya nyongeza ya mshahara. Hawa ndio watu wanaomba hili Bunge la Seneti liwasaidie ili wapate malipo yao. Nikiwa katika Kamati ya Bunge la Seneti ya Elimu ama Standing Committee on Education, tutalivalia njuga ili tuangalie ya kwamba hawa walimu ambao wamestaafu na wengine wengi vile Sen. M. Kajwang amesema, wengine washaa kufa tayari, ili wapate hiyo nyongeza, walipwe pesa yao na familia zao pia zipatwe kulipwa. Imekuwa mtindo wa Serikali ya Kenya kutolipa wananchi wao pesa zao wakati zinahitajika. Katika hili Bunge, kuna Statement imeletwa na Sen. (Dr) Murango kuhusu makansela amabao wamestaafu na hawajapata kulipwa pesa zao. Hili ni swala ambalo tuliliangalia nikiwa Naibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Leba katika Bunge lililopita. Tulielekea mpaka kwa Mhe. Ukur Yatani ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na akaahidi ya kwamba katika bajeti, kutawekwa pesa za kulipa hawa makansela. Mpaka leo, hawa makansela hawajalipwa. Ni vizuri Serikali iheshimu wananchi wake na kuwalipa pesa zao za takrima wakati wanapozihitaji. Huo ndio utakuwa mchango wangu. Tutalivalia njuga hili swala ili hawa walimu pamoja na makansela walipwe pesa zao kwa wakati unaofaa. Asante sana, Bw. Spika."
}