GET /api/v0.1/hansard/entries/1219415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219415,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219415/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante sana, Mstahiki Spika. Ninampa kongole Mwenye Ardhilhali aliyeomba kuhusu malipo ya uzeeni na nyongezo ya mishahara ya walimu. Ni kitu kinafaa kuzingatiwa kwa maana kwa muda mrefu mambo yanayokumba waalimu mengi hayajakuwa ya kutia moyo sana. Ya kwanza, kuna uhawilisho ambao umekuwa ukiendelea; kupelekwa eneo tofauti na bado wanalipwa mishahara ile ile. Kwa hivyo, ni vizuri hiyo nyongeza izingatiwe na ada ya walimu pia iangaliwe. Nilikuwa nimeomba Ardhilhali ambayo ilienda kwa Kamati ya Leba na Maslahi ya Jamii kuhusu malipo ya wale madiwani waliokuwepo. Ni vizuri pia ile izingatiwe kwa sababu tunapokaa sana bila kuwalipa halafu tunalipa wakati miaka imesonga sana ni sawa tu na kumpatia mtu wembe ama kichana wakati ana na kipara kama mimi hapa. Haitakuwa na maana yeyote kwa mtu ambaye kwa maisha yote amekuwa akitaabika kwa kungojea zile fedha."
}