GET /api/v0.1/hansard/entries/1219438/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219438,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219438/?format=api",
"text_counter": 60,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Imekuwa shida. Kwa hivyo, naunga mkono mwalimu aangaliwe mambo yake. Kama ilivyofanyika mwaka uliopita, walimu walipigwa transfer na pia wakatenganishwa na familia zao. Wakati serikali ya Kenya Kwanza ilipata mamlaka iliapa kuwarudisha walimu Hao kwa shule zao na ikawa haijafanyika. Kulipaswa kuwa na mkutano mkubwa wa walimu ulioandaliwa na Kamati ya Elimu ya Seneti. Lakini jambo la ajabu ni kuwa waandalizi hawakuhudhuria kikao hicho. Kwa hivyo, mwalimu anaendelea kunyanyaswa. Ningeomba hatua ichukuliwe ili kuonekana kutakuwaje. Walimu wale wako Kitui, Tharaka-Nithi na wanatoka Embu, hawajarudishwa Embu. Imekuwa ni shida. Shida hiyo haiko Embu peke yake, iko katika kaunti arobaini na saba. Bunge ina mamlaka ya kuangalia vile Wizara ya Elimu itabadilishwa ili waweze kufanya kazi vizuri. Kuongezea, departments zote zijue kuwa mkubwa anapoitwa na Seneti, anafaa ahudhurie kikao. Kwa hivyo, ninaomba Seneti ichukulie hatua wale watu ambao hawatatii wito wa kamati za Seneti. Asante."
}