GET /api/v0.1/hansard/entries/1219473/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219473,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219473/?format=api",
    "text_counter": 95,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Nataka kuchukua muda huu kusema ya kwamba ninaunga mkono mjadala huu. Leo ni sadfa kwa sababu leo ni siku ya wanawake ulimwenguni na tena siku ya leo ndio jina lake limeletwa hapa. Hii inamaanisha ya kwamba yeye akiwa kama mwanamke na kulingana na vile imesemekana amebobea katika kazi yake. Akikuwa Naibu wa Gavana wa Benki Kuu ya Kenya anafaa atilie mkazo kwa sababu wakati huu kama Serikali tunapitia majanga mazito kwa sababu watu wengi wako na shida. Ni juzi tu tumesikia ya kwamba Serikali iliyokuwepo walikuwa wakipigia watu simu wakiwaambia ni mpaka wafanye hivi na vile vingine. Mimi nina hakika ya kwamba Dr. Susan, yeye ni jasiri, hatapokea simu ambazo hazipaswi kuwa zikimfanyisha kazi yake. Yeye afuate sheria zilizowekwa katika Jamhuri ya Kenya. Kuna mazoea ya watu wengine kuwapigia wengine simu lakini ninajua ya kwamba Serikali yetu ya Kenya Kwanza haitakuwa na ule mtindo. Tumesema vizuri ya kwamba mtu afanye kazi kwa mujibu wa sheria iliyowekwa. Nina hakika ya kwamba Dr. Susan atafanya ile kazi kwa ujasiri. Kwa vile yeye anaingia katika Benki Kuu ya Kenya na hao ndio wanaoshughulikia pesa, akumbuke ya kwamba tumezungumzia hapa kinaga ubaga kuhusu waalimu na shida wanazopitia. Sio walimu peke yao, hata madiwani wamekuwa wakipitia katika janga hili. Tumelivalia njuga, tumeliongea lakini jambo hili linatakiwa kutiliwa maanani. Kwa sababu yeye atakuwa anashughulikia mambo ya fedha, waangalie na waone ya kwamba walimu na madiwani ambao wamestaafu wamelipwa pesa zao. Watu wengi wanakuwa wafisadi wanapofanya kazi kwa sababu wanahofia wakistaafu hawatalipwa pesa zao. Wanafuatilia wimbo ambao umeimbwa na Samba Omar Mapangala ati “Vunja mifupa kama meno ingali ipo”. Unapata mtu anaanza"
}