GET /api/v0.1/hansard/entries/1219541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219541,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219541/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika. Nimesimama kuambatana na Kifungu cha 52(1) cha Kanuni za Kudumu za Seneti kuzungumzia swala la dharura ambalo ni kuzuiliwa ama kukatwa kwa umeme katika Hospitali Kuu Ya Pwani, yaani Coast General Hospital, hapo jana, tarehe 7, Machi, 2023. Bw. Spika, hospitali hii ndiyo taasisi kubwa ya afya katika eneo zima la Pwani. inahudumia Mombasa, Kwale, Kilifi, Tana River, Lamu na Taita Taveta. Kwa hivyo, utendakazi wake unaangaziwa Pwani nzima Kwa jumla. Kudorora kwa huduma katika hospitali hii kutasababisha maafa kwa wengi ambao tegemeo lao ni hospitali hii. Bw. Spika, kuna huduma muhimu katika hospitali hii zinazoendeshwa na vifaa vya umeme, kama vile vyumba vya wagonjwa mahututi, vitanda vya watoto wachanga waliozaliwa kabla ya wakati, huduma za picha na vile CT Scan . Bw. Spika, ni kosa la jinai kwa Kampuni ya Umeme, kukata umeme kwa taasisi kama hospitali. Maafa yoyote yatakayotokea itakuwa ni jukumu la wakurugenzi wa kampuni hiyo kujibu mahakamani. Kwa hivyo, inapaswa swala hili liangaziwa kwa haraka, ili waliosababisha kukatwa kwa umeme wachukuliwe hatua, ili iwe funzo kwa wengine. Bw. Spika, hivi majuzi, hospitali hii imekuwa katika vyombo vya habari kutokana na kifo cha kijana wa miaka 17, Emmanuel Chiringa, kutoka eneo la Mwele, Rabai, Kaunti ya Kilifi, ambaye alikuwa amelazwa hospitalini humo baada ya kudungwa chanjo dhidi ya Korona alipokuwa shuleni. Kijana huyu alikuwa amesubiri matibabu kwa siku kadhaa kabla ya kufariki. Bw. Spika, malalamiko ya madaktari yamekithiri, huku wengine wakisimamishiwa mishahara wakati wako kwenye mafunzo yao na wengine kuzuiliwa kuanza kazi baada ya kumaliza mafunzo. Bw. Spika, vile vile, kuna kuharibika mara kwa mara kwa vifaa muhimu kama vile CT-Scan na vifaa vinginevyo ambavyo husababisha wagonjwa kukosa huduma."
}