GET /api/v0.1/hansard/entries/1219547/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219547,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219547/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii, ili niweze kuunga mkono Taarifa iliyosomwa na Seneta wa Mombasa. Kusema kweli, ni jambo la kusikitisha kwa Kenya Power kukata umeme katika Hospitali Kuu ya Pwani. Kaunti za Pwani kama vile Kwale, Kilifi, Malindi, Tana River na Lamu zinategemea hospitali hii. Ukiangalia kwa undani, nalaumu sana Kenya Power. Mwaka juzi kabla twende kwenye uchaguzi, sehemu za Kombani, Kwale, waliambiwa mapema kwamba, kuna nguzo iliyoanguka chini na italeta athari ya mtu kufa. Waliwacha mpaka mtoto akapita, akakanyaga hiyo kitu na wakafariki akiwa na mama yake, kwa sababu ya kupuuza. Leo, tunaskia wamekata umeme katika Hospitali ya Makadara. Hili ni jambo ambalo kiongozi yeyote atakaye simama hapa hatakubaliana nalo. Kwa hivyo, wale waliofanya kitendo hicho, awe afisa, meneja au mkurugenzi wa umeme katika sehemu ya Pwani, ajue kwamba siku moja, baba, mtoto au ndugu yake atakuwa mgonjwa na ataenda katika hospitali hiyo ya Pwani. Tunakemea jambo hilo."
}