GET /api/v0.1/hansard/entries/1219551/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219551,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219551/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Thang’wa",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Najiunga na wenzangu kuunga mkono Taarifa iliyoletwa na Seneta wa Mombasa, Sen. Faki. Bw. Spika, tungetaka wao wenyewe wafike mbele ya Kamati ambayo utapatia kazi kuchunguza swala hili ili watuelezee kwa nini wao hawana utu wa kujua kwamba hospitali ni sehemu ambayo inahitaji umeme kila siku. Kama tunafanya hivyo, ni vizuri pia Kaunti, sana sana magavana, watafute njia mbadala ambayo itasaidia hizi hospitali kuwa na umeme wa kujisimamia. Mahali kama Mombasa, najua mambo ya Solar ama kutumia jua inahitajika. Najua Gavana mwenyewe akijua hospitali yake vile ilivyo, itabidi waweke kwenye bajeti pesa ya kununua solar . Hata kama sio hospitali yote, katika kile chumba cha watoto wanaweza tumia solar, ndio wale watu wa Kenya Power, kwa sababu hawana utu, wakifanya kitu kama hicho, Gavana mwenyewe atakuwa amefanya jambo la kusaidia watu wake waliomchagua. Nakumbuka wakati Rais William Ruto, alikuwa anatoa hotuba yake katika Bunge zote mbili wakati alipochaguliwa, alisema watakubalia vijana, akina mama na watu wengine kutengeneza vikundi vyao kwa jina lingine Cooperatives. Wale ambao wanaweza kutengeneza umeme kupitia maji, jua au njia nyingine yeyote, watapatiwa nafasi wawe wakiuzia Serikali ule umeme ama stima. Ningeomba serikali za kaunti, hata kama tunalaumu wale ambao hawana utu, hatuwezi kuwa tukilia kila siku. Kila siku asubuhi tunaamka kulaumu huyu au yule. Sisi wenyewe tunayo kaunti kule mashinani, zinafanya nini? Hata kama stima imezimwa, hakuna kitu ama mtu amezuia gavana wa kaunti yeyote kuanzisha kampuni yake ya umeme katika zile hospitali ili tuwache kuilaumu Kenya Power. Bw. Spika, kabla hawajapata ule utu, tuangalie vile sisi kama Seneti, vile tunaweza washurutisha magavana kabla hatujapitisha pesa zao. Tunaweza kusema lazima wachukuwe hatua kuhakikisha kuna umeme, maji na pia barabara za kupitia kwenda hospitali, ili ambulansi ama piki piki zikipeleka watu hospitali, waweze kufika vizuri. Hata hivyo, naunga mkono hiyo Statement ya Sen. Faki. Lazima Kenya Power wafike mbele ya hiyo Kamati. Wakati huu wasitume wawakilishi. Wafike wenyewe ndio wajibu swala hilo. Asante sana, Bw. Spika."
}