GET /api/v0.1/hansard/entries/1219556/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219556,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219556/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "na kadhalika. Wale ni watu ambao kwamba hawana hatia. Kwa nini waathirike kulingana na kitendo cha Kenya Power? Kwa hivyo, Kenya Power inapoenda kukata umeme, ni muhimu wazingatie ile sehemu wanayoenda kukata umeme, ni wangapi wataathirika kwa kile kitendo ambacho watatekeleza. Kukatia mtu umeme kwa nyumba au sehemu za biashara ni kitendo ambacho kinaeleweka. Lakini kukata umeme katika sehemu kama hospitali ni lazima wawe na mpango maalum wa kuweza kupeana notice ya kutosha ama kudhibiti umeme kwa sababu ya wale waathiriwa ambao wataathirika kwa kile kitendo chao ambao hawana hatia ya wao kuathirika kulingana na kukatwa kwa umeme. Pia naunga mkono Mheshimiwa alivyosema kwamba kuna umuhimu kuwe na mbinu mbadala ya kuweza kuwa na umeme mbadala badala ya kutegemea Kenya Power. Kenya Power kwa sababu ni monopoly, wanajaribu sana kutesa watu hapa nchini. Unabandikwa bills kubwa kubwa, huna njia ni lazima ulipe. Wananchi na wafanyi biashara wanalipa mabill makubwa makubwa. Wananchi wanalipa ushuru karibu mara mbili au tatu. Unalipa ushuru wa nchi na Kenya Power. Kwa hivyo Kenya Power ni lazima iwe na mipangilio ya kukosa kungandamiza mwananchi, kwa sababu hawana njia ni wao pekee yao ambao wanafanya hiyo shughuli. Kwa hivyo, mimi naunga mkono na ninasema kwamba ni lazima hatua ya dharura ichukuliwe dhidi ya wale ambao wamefanya kitendo kama hicho. Hii ni kwa sababu wameadhibu watu ambao hawana hatia. Asante, Bw. Spika."
}