GET /api/v0.1/hansard/entries/1219557/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1219557,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219557/?format=api",
"text_counter": 179,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante sana Bw. Spika. Yale ambayo tunajadili sasa, kwangu mimi ni kidonda ambacho kimekuwepo katika kaunti za humu Kenya kwa sababu, iwapo serikali za kaunti zinajua kwamba kuna pesa za umeme ambazo lazima zilipwe. Kwenye bajeti ama katika usimamizi wa hospitali, lazima wawe wanajua kwamba gharama ya umeme ni pesa fulani na iwapo hakuna umeme katika zahanati ama hospitali hizo ni yapi yapaswa kufanywa kuhakisha ya kwamba kuna umeme? Katika hospitali zakibinafsi wako na transformer . Pia, wako na mashini za kusaidia vyumba vya wagonjwa mahututi na vyumba vya upasuaji, kuhakikisha kwamba kuna umeme katika hospitali hizi. Nimefanya utafiti kidogo huko nyuma na nikagundua kwamba zile pesa ambazo kidogo kidogo hutozwa wagonjwa na kuwa na hazina katika hospitali, baadhi ya magavana wametoa hizo pesa kuenda kwenye kibindo kikubwa cha kaunti. Hivi kwamba kulemaza uwezo wa madaktari katika hospitali kugharamia umeme na mambo madogo madogo ambayo yanaweza okoa maisha ya Wakenya. Sasa, Kamati ya Afya katika Seneti lazima tuangalie mfumo wa kiuchumi ambao utasaidia hospitali kuu katika kaunti zetu kujisamamia na kuhakisha kwamba hakuna kupoteza maisha kutokana na ubadirifu wa pesa ama uzembe wa magavana katika kaunti. Vile vile, swala hili linaangazia mstakabali kati ya shirika la umeme na taasisi mbali mbali za serikali. Msimamizi wa Shirika La Umeme Mombasa, lazima awe na"
}