GET /api/v0.1/hansard/entries/1219559/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1219559,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1219559/?format=api",
    "text_counter": 181,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "heshima na kumtafuta gavana ama msimamizi wa kiwanda ama hospitali na kumueleza; ndugu yangu siku zimefika na lazima ulipe deni. Una mpango gani wa kulipa? Wakubaliane ili pasikuwe na shida ama kupoteza maisha ya watu. Mimi naunga mkono Hoja ambayo ndugu yangu Sen. Faki ameleta. Lakini katika Kamati ya Afya, lazima twende pale mashinani na tuhakikishe kwamba mifumo ya fedha, umeme na kugharamia umeme wa kushughulikia mashine mbali mbali katika nchi hii yasisimamishwe kwa sababu ya pesa. Mwisho, tukiendelea hivi, utasikia Shirika la Umeme limekata umeme katika kituo cha polisi. Ikikata umeme katika maeneo ya usalama, hapa ni kuwapa majambazi nafasi ya kutawala miji yetu. Sasa ni lazima tuwe na mfumo wa mstakabali kuhakisha kwamba serikali na Shirika la Umeme zinongee ili Wakenya watoza ushuru wasihangaike na kufa kwa makosa ambayo sio yao. Asante sana, Bw. Spika."
}